Skip to main content

MWANAMKE WA SIKU; SAMIA SULUHU HASSAN

Samia Suluhu Hassan

Ushindi wa John Pombe Magufuli wa CCM umetoa fursa kwa Bi Samia Suluhu Hassani kuhudumia taifa hilo la Afrika Mashariki kama mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa rais wa Tanzania.

Lakini Bi Samia ni nani?
Tangu kongamano la Chama tawala nchini Tanzania CCM kumteua Daktari John Pombe Magufuli Joseph kuwa mshika bendera wa CCM, Chama hicho kiliweka historia kwa kumteua Bi Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza.

Tangu Dodoma, Bi Samia aliwekwa kwenye ramani ya wanasiasa wanawake waliobobea barani Afrika.

Lakini Bi Samluia Suhu Hassanni Nani ?
Bi Samia Suluhu ana umri wa miaka 54. Kwa wale wanaomjua Bi Samia wanasema kuwa ni mchache wa maneno. Asili yake ni Kisiwani Zanzibar. Bi Samia Suluhu Hassan amewahi kushikilia nyadhifa za uwaziri katika serikali ya Muungano wa Tanzania na kadhalika amewahi kutumikia serikali ya visiwani Zanzibar kama waziri katika afisi ya makamu wa rais.
Ni mwanamke wa Kwanza kuwa Mgombea Mwenza

Tangazo la kumtaja kama mgombea mwenza wa rais mteule wa tano wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania sasa limezaa matunda na kumuweka Bi Samia katika mstari wa mbele barani Afrika kama naibu rais wa Jamhuri ya Tanzania.

Chama CCM pia kimeingia katika daftari la vyama vilivyowapa wanawake sauti katika serikali yake katika karne hii ya 21.

Bi Samia alikamilisha masomo ya shule ya upili mwaka wa 1976 .
Masomo

Aliajiriwa kama mchapishaji katika wizara ya mipango na maendeleo ya nchi, kazi ambayo aliifanya huku akiendelea na masomo yake hadi alipohitimu katika chuo kikuu cha Manchester, Uingereza.

Bi Samia anasema kuwa njia yake ya ufanisi haijakuwa rahisi kama inavyodhaniwa.

''Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija.''

Kimsingi ufanisi wangu katika siasa za Tanzania umetokana na uweledi na umakini katika kila jambo ninalolifanya.''

''Sio rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi," anasema Bi Samia.

Familia
Aliolewa mwaka wa 1978, kwa Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo .

Walijaliwa watoto wanne.
Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir (1982), ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar

Siasa
Alijiunga na siasa mwaka wa 2000.
Wakati huo alijiunga na bunge la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum.

Haikuchukua muda nyota yake ikaanza kung'aa na akateuliwa kuwa waziri na rais Amani Karume.

Alitumikia taifa hadi mwaka wa 2005 alipochaguliwa tena na kuteuliwa upya kama waziri.

Mwaka wa 2010 alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi.

Punde tu akateuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano.

Wadhifa aliohudumu hadi RAIS MTEULE Dkt John Pombe Magufuli alipomtangaza kuwa mgombea mwenza.

Chanzo : BBC Swahili

Comments

Popular posts from this blog

KIJANA WA SIKU; PAUL MAKONDA

PAUL MAKONDA Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda. Hii ni historia ya muheshimiwa paul makonda mkuu wa mkoa jijini Dar es salaam, amezaliwa tarehe 15\2\1982 huko Kolomije wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza katika zahanati ya Kolomije siku ya Jumatatu saa 1;30 Asubuhi ni mtoto wa kipekee wa kiume katika familia ya mzee Makonda na bi.Suzan mh.Paul Makonda ametoka kwenye familia ya kawaida mama yake alisoma mpaka darasa la 7 na baba yake hakusoma kabisa lakini pia alihishi katika kusudi la mungu na kumtumikia pia ni kitu kilichomfanya awe bora katika ukuaji wake wakati wote, alibahatika kuwa na ndugu  wa kike lakini aliweza kuishi ndani ya mwaka na nusu toka kuzaliwa kwake na kufariki dunia.  Amesoma shule ya msingi katika shule ya kolomije,sekondari alisoma kutokana na changamoto za kipato katika familia hakuweza kwenda kidato cha tano na kwenda chuo Mbegani chuo cha uvuvi mjini bagamoyo kuanza ngazi ya cheti,diploma na ata kufika chuo kikuu ka...

KIJANA WA SIKU:MARK ZUCKERBERG

MJUE MARK ZUCKERBERG MGUNDUZI WA FACEBOOK aka KITABU USO...!!! Bio , Facebook , Mark Zukerberg Ni Muyahudi mkazi wa Marekani Aliacha masomo Havard baada ya kulamba utajiri Na Blogger team, Andrew Chale,Tanzania MTANDAO wa Facebook uligunduliwa na mwanafunzi wa masomo ya sayansi wa Chuo Kikuu cha Harvard, Mark Zuckerberg, akishirikiana na wanafunzi wenzake, Eduardo Saverin, Dustin Moskovitz na Chris Hughes. Mwanzo wa jina la mtandao ndio ulizaa historia ya Facebook. Mtandao huo awali ulifahamika kama Facemash. Zuckerberg alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili alipoandika ‘software’ ya mtandao wa Facemash. Endelea kusoma kwa kubofya hapo chini Continue Reading>>>>>> Alitumia maarifa yake ya sayansi ya kompyuta vizuri kwa kuingia katika mtandao wa usala...

MWANAMKE WA SIKU:ASHA ROSE MIGIRO

       Tarehe 1 Februari mwaka 2007 ni tarehe ambayo Dr.Asha-Rose Mtengeti Migiro hawezi kuisahau kirahisi. Hii ndiyo siku alipokabidhiwa rasmi ofisi na majukumu ya unaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa cheo ambacho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997 kilikuwa hakijawahi kushikiliwa na sio tu na mwanamke yeyote mweusi bali pia mwafrika yeyote. Kwa maana hiyo Dr.Asha-Rose Migiro ndiye mwanamke wa kwanza mweusi kushikilia wadhifa huo na pia mwafrika wa kwanza. Mwanamke mwingine ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kushikilia cheo hicho alikuwa ni mzungu raia wa Canada Louise Frechette ambaye alianza kukitumikia cheo hicho mapema mwaka 1998. Dr.Migiro anayo historia nyingine ya kujivunia. Yeye ndio alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania tangu nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961. Aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 2006. Hivi leo Dr.Asha Rose Migiro ambaye ni mke wa Professa Cleophas Migiro na pia mama wa watoto w...